Zaburi 96:13
Mbele za BWANA, kwa maana anakuja, kwa maana anakuja aihukumu nchi, atauhukumu ulimwengu kwa haki, na mataifa kwa uaminifu wake.
Kuna maefu ya madhehebu mbalimbali ulimwenguni leo. Kila dini inaihukumu nyingine, hata hivyo zote zinaahidi wokovu kupitia kwa dhehebu lao. Tunajuaje tuchague lipi?
Kama tukichagua kanisa Katoliki, basi tunaukubali upatanisho wa watakatifu, ambao si zaidi ya kuomba sanamu. Biblia inasema, “Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu ni mmoja, Mwanadamu Yesu Kristo,” (I Tim. 2:5). Padri anaitwa “Baba” jambo ambalo lilikatazwa na Yesu katika Mat. 23:9: “Wala msimwite mtu baba duniani; maana baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni.” Assemblies of God inatwambia ya kwamba kunena kwa lugha ndilo thibitisho la kwanza la Roho Mtakatifu, wakati Paulo alisema, “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.” (I Kor 13:1)
Karibu madhehebu yote ni wepesi kutuambia ya kwamba mambo mengi katika Biblia yamefasiriwa vibaya, yalipotea katika kufasiriwa, ama hayatumiki katika ulimwengu wa sasa. Kwa hiyo, je! inatupasa kuiamini Biblia ama mafundisho ya kimadhehebu? Mungu atatumia kitu gani kama kipimo cha hukumu?
Kama ningemwuliza Mkatoliki hapa usiku wa leo, “Je! unafikiri Mungu atauhukumu ulimwengu kwa kitu gani?” Mkatoliki atasema, “Kwa Kanisa Katoliki.” Vema, sasa, ni Kanisa lipi la Katoliki? Sasa wana la Kirumi, la Othodoksi ya Kiyunani, na mengi yao. Lingekuwa ni Kanisa lipi la Katoliki? Mlutheri anasema, “Kwa sisi,” basi wewe Mbaptisti mko nje. Halafu basi kama sisi tungesema, “Kwa Baptisti,” basi ninyi Wapentekoste mko nje. Kwa hiyo kungekuwako na utata mwingi, hakuna mtu angejua la kufanya; kwa hiyo Yeye kamwe hakuahidi kuuhukumu ulimwengu kwa kanisa.
Yeye aliahidi kuuhukumu ulimwengu kwa Kristo, Naye Kristo ni Neno. Na Biblia ndiyo itakayouhukumu ulimwengu, ambayo ni Yesu Kristo yeye yule jana, leo, na hata milele.
Marejeo
Yohana 1:1
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
Yohana 1:14
Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee, atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli.
Yohana 5:22
Tena Baba hamhukumu mtu yeyote, bali amempa Mwana hukumu yote:
Yohana 12:48
Yeye anikataaye mimi, asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye; neno hilo nililonena, ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.
Waefeso 1:5-7
Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake.
Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo mpendwa.
Katika yeye, tunao ukombozi kwa njia ya damu yake, yaani, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.
Waefeso 2:5-8
Hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema.
Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu;
Ili katika zamani zinazokuja adhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu.
Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu.
I Yohana 1:7
Bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi zote.
Ufunuo 22:18-19
Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu yeyote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.
Na mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.